Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:12

Marekani yaihakikishia Ukraine msaada wake kwa vita dhidi ya Russia


Waziri wa ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, Jumanne amesema anatarajia Ukraine kufanya mashambulizi mapya ya kijeshi katika msimu wa machipuko.

Mashambulizi hayo ni kukabiliana na mashambulizi ya Russia, huku akiihakikishia serikali ya Kyiv kwamba Marekani na washirika wake wa magharibi bado wapo madhubuti katika ahadi zao za juhudi za kivita.

Akiwa katika mkutano wa NATO uliokutanisha mawaziri wa ulinzi kujadili uratibu wa misaada ya kijeshi kwa Ukraine, amesema hayo Kremlin bado inadhani itapata ushindi kwa kudhani kuwa tutachoka.

Silaha zaidi zinaendelea kutumwa siku kwa siku, lakini Kyiv inatoa mwito kwa serikali za magharibi kutuma ndege zake za kisasa zaidi za kivita, kitu ambacho mataifa hayo yanaendelea kutafakari kufanya hivyo.

Aliongeza kusema licha ya hayo, hakuwa na tangazo lolote kwa siku ya Jumanne.

XS
SM
MD
LG