Wizara ya fedha ya Marekani imesema katika taarifa kwamba haina mpango wa kutoa leseni mpya ili kuiruhusu Russia kuendelea kuwalipa wakopeshaji wake kupitia benki za Marekani.
Tangu awamu ya kwanza ya vikwazo, wizara ya fedha ya Marekani ilizipa benki leseni ya kushughulikia malipo yoyote ya dhamana kutoka Russia. Muda wa fursa hiyo unakamilika saa sita usiku Mei 25.
Kumekuwa pia ishara kwamba utawala wa Biden hauna niya ya kuongeza muda huo wa kikomo.
Bila leseni ya kutumia benki za Marekani kulipa madeni yake, Russia haitakuwa na uwezo wa kulipa dhamana za wawekezaji wake wa kimataifa.
Kremlin imekuwa ikitumia Benki ya JPMorgan Chase na Citigroup kama njia ya kulipa madeni yake.