Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:21

Marekani yaeleza wasi wasi kuhusu ujenzi barabara Serengeti.


Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete .
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete .

Waziri mdogo wa mambo ya nje wa Marekani Johnnie Carson ameeleza wasi wasi wa serikali ya nchi yake kuhusu ujenzi wa bara bara kwenye mbuga ya Serengeti na kuzungumza na viongozi wa Tanzania.

Waziri mdogo wa mambo ya nje ya Marekani anayeshughulikia maswala ya Afrika, Johnie Carson, ameelezea wasi wasi juu ya mipango ya serikali ya Tanzania kujenga barabara kupitia hifadhi ya mbuga ya Serengeti.

Wanamazingira wana wasiwasi kuwa barabara hiyo itaaathiri kuhama hama kwa wanyama kama vile nyumbu kuelekea kwenye hifadhi za Kenya.

Waziri Carson alisema Jumatano kuwa amewahi kuzungumzia suala hilo na waziri wa mambo ya nje wa Tanzania na pia Rais Jakaya Kikwete. Carson amesema wanajua vizuri kuhusu wasi wasi huo na wanajua thamani ya maisha ya wanyama pori na Serengeti.

Mwanadiplomasia huyo wa Marekani amesema anaelewa kuwa viongozi wa Tanzania wanatafuta njia za kuboresha uchumi wa nchi yao na kwamba hawana nia ya kuharibu mbuga hiyo maarufu.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton anategemewa kukutana na rais Kikwete wakati wa ziara yake Tanzania wiki ijayo.

XS
SM
MD
LG