Rais Barack Obama wa Marekani, Jumatatu, ameweka shada la maua kwenye kaburi la mwanajeshi asiyejulikana wakati wa hafla ya kumbukumbu iliyofanyika kwenye makaburi ya kitaifa yaliyo kwenye Bustani Arlington jimbo la Virginia.
Rais huyo alikuwa na shughuli nyingi zilizoratibiwa wakati wa kuadhimisha sikukuu ya Memorial Day, inayowaenzi wanaume na wanawake waliofariki dunia wakihudumu katika jeshi la Marekani.
Kabla ya hafla hiyo, Rais Obama alikuwa mwenyeji wakati wa kifungua kinywa kwenye ikulu ya white House, kwa makundi ya wanajeshi wakongwe na viongozi wa ngazi za juu wa kijeshi.
Baada ya kuweka shada la maua, Obama aliwahutubia waliohudhuria hafla hiyo.
Marekani huadhimishwa sikukuu hiyo kila Jumatatu ya mwisho ya Mwezi Mei, na hii ndiyo hafla ya mwisho ya Memorial Day kuhudhuriwa na Obama akiwa rais wa Marekani.