Marekani na Pakistan zimehitimisha mazungumzo yao ya hivi karibuni ya kupambana na ugaidi na kukubaliana kuimarisha ushirikiano wao katika mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi kama vile Pakistan Taliban, na mshirika wa kikanda Islamic State.
Washington na Islamabad walitoa taarifa ya pamoja wakati huo huo Jumatatu, wakisema mazungumzo ya nchi mbili ya Mei 10 yaliyoandaliwa na Marekani yalijikita katika kukabiliana na changamoto kubwa zaidi kwa usalama wa kikanda na ulimwengu.
Mkutano huo umekuja wakati kukiwa na ongezeko la ugaidi nchini Pakistan, na kusababisha vifo vya mamia ya watu, ikiwemo vikosi vya usalama. Ghasia hizo zinadaiwa kufanywa na kundi la Tehrik-i-Taliban Pakistan (TTP), linalojulikana kama Pakistan Taliban, ambao wanaaminika kufanya kazi kutoka katika maeneo ya hifadhi katika nchi jirani ya Afghanistan.
“Pakistan na Marekani zinatambua kuwa ushirikiano wa kupambana na ISIS-Khorasan, TTP, na taasisi zingine za kigaidi utaendeleza usalama katika kanda hiyo na kutumika kama mfano wa ushirikiano wa nchi mbili na kikanda kushughulikia vitisho vya ugaidi vya kimataifa”, taarifa hiyo ilieleza.
Forum