Rais Joe Biden hivi karibuni alizungumzia kisa hicho akidhihirisha hasira yake juu ya uamuzi wa mahakama ya juu ya Marekani kubatilisha haki ya kutoa mimba nchini kote.
Gerson Fuentes alikamatwa Jumanne, kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, na kufikishwa mahakamani Jumatano katika kaunti ya Franklin, mahakama ya wilaya.
Polisi wamesema, inaonekana Fuentes, mwenye umri wa miaka 27 alikuwa anaishi nchini Marekani kinyume cha sheria, na alikiri kumbaka msichana huyo mara mbili, mchunguzi wa polisi ametoa ushahidi mahakamani.
Fuentes anashikiliwa kwa dhamana ya dola milioni 2 na atasikilizwa katika kesi ya awali Julai 22.
Muathiriwa alifanyiwa operesheni ya kutoa mimba mjini Indianapolis tarehe 30 Juni, kulingana na ushahidi wa afisa huyo wa polisi.