Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:16

Marekani kutuma Ukraine mfumo wa kisasa wa kunasa makombora


Ndege ya kivita ikiwa katika mazoezi
Ndege ya kivita ikiwa katika mazoezi

Marekani inapanga kuisaidia Ukraine na vifaa vya kivita vya ulinzi wa angani, vyenye uwezo wa kunasa makombora.

Mfumo huo kwa jina HAWK, unalenga kuilinda Ukraine dhidi ya mashambulizi ya makombora ya Russia.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba mfumo huo wa ulinzi ni nyongeza ya mfumo ambao Marekani ilipeleka Ukraine awali, wenye uwezo wa kunasa makombora ya masafa mafupi.

Utawala wa rais Joe Biden utatumia mamlaka ya rais kutuma mfumo huo wa ulinzi pasipo idhini ya bunge.

Rais wa Marekani ana mamlaka ya kutuma au kubadilisha huduma za ulinzi pasipo idhini ya bunge kama kuna hali ya dharura.

Haijabainika kuhusu idadi ya mifumo hiyo ya kunasa makombora, itakayopelekwa Ukraine.

Rais wa Marekani Joe Biden, aliahidi rais wa Ukraine msaada zaidi wa silaha za kisasa, baada ya Russia kuishambulia Ukraine kwa makombora kadhaa mwezi huu na kusababisha uharibifu mkubwa.

Katibu mkuu wa muungano wa NATO Jens Stoltenberg, amesema kwamba Spain imeahidi msaada za mfumo wa kunasa makombora, HAWK.

Marekani imetoa msaada wa dola bilioni 17.6 kwa Ukraine kwa ajili ya silaha, tangu Russia ilipoivamia nchi hiyo kijeshi, Februari 24.

XS
SM
MD
LG