Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 01:57

Marekani kutoa pipa milioni 1 za mafuta kwa siku kukabiliana na bei ghali ya bidhaa hiyo.


Ishara inaonyesha bei ya petroli nje ya kituo cha mafuta huku bei zikiongezeka, Washington DC, Machi 8, 2022. Picha ya AFP
Ishara inaonyesha bei ya petroli nje ya kituo cha mafuta huku bei zikiongezeka, Washington DC, Machi 8, 2022. Picha ya AFP

Rais wa Marekani Joe Biden Alhamisi ametangaza kwamba pipa milioni 1 za mafuta zitatolewa kutoka kwa hifadhi ya mafuta ya Marekani kila siku kwa kipindi cha miezi sita ili kusaidia kupunguza bei ya mafuta ambayo imekuwa ghali sana kwa waendesha magari wa Marekani.

Biden amesema mapipa milioni 180 kutoka ghala hilo la mafuta linalotumiwa wakati wa dharura, zitasaidia kukabiliana na athari za uvamizi wa Ukraine ulioamrishwa na rais Vladmir Putin kwenye soko la kimataifa la mafuta.

“Bei zetu za mafuta zinaongezeka kutokana na vitendo vya Putin. Hakuna usambazaji wa kutosha wa mafuta. Na kikomo ni kwamba, ikiwa tunataka kupunguza bei za mafuta, tunahitaji usambazaji wa kutosha wa mafuta sasa hivi.”

Baadhi ya wataalamu wa masuala ya nishati wanasema mafuta hayo kutoka kwenye hifadhi hayatapunguza vya kutosha athari za bei ghali ya mafuta kwenye soko la kimataifa.

Na wabunge wa chama cha Republican wanadai sera kuhusu nishati za utawala wa Biden ndizo zakulaumiwa kutokana na gharama kubwa ya mafuta na gesi badala ya vitendo vya rais wa Russia.

XS
SM
MD
LG