Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:31

Marekani kuonya China kuhusu makombora ya Korea kaskazini


Kombora la Korea kaskazini likipaa angani kutoka sehemu isiyojulikana ndani ya Korea kaskazini January 1, 2022
Kombora la Korea kaskazini likipaa angani kutoka sehemu isiyojulikana ndani ya Korea kaskazini January 1, 2022

White House imesema kwamba rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kumuonya mwenzake wa China Xi Jinping kwamba hatua ya Korea Kaskazini kuendelea kuimarisha uwezo wake wa silaha itapelekea Marekani kuongeza wanajeshi wake katika eneo hilo.

Biden anatarajiwa kukutana na Jinping jumatatu wiki ijayo katika kongamano la viongozi kutoka nchi tajiri 20 tajiri zaidi duniani, G20, mjini Bali, Indonesia.

Marekani ina wasiwasi kwamba Korea Kaskazini inapanga kuanza tena utengenezaji wa bomu la nyuklia, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2017.

Marekani inaamini kwamba China na Russia wana uwezo wa kuishawishi Korea kaskazini kuachana na mipango yake ya kutengeneza silaha za nyuklia.

Mshauri wa usalama wa taifa Jake Sullivan, amesema kwamba Biden atamueleza rais wa China kwamba Korea Kaskazini ni tishio sio tu kwa Marekani na washirika wake kama Korea Kusini na Japan, lakini kwa usalama wa eneo hilo lote.

Vikwazo vinavyoongozwa na Marekani dhidi ya Korea Kaskazini vimeshindwa kuizuia Korea Kaskazini kuendelea na mipango yake ya kutengeneza silaha na kufanya majaribio ya makombora yakiwemo ya masafa marefu.

Biden amekutana na viongozi wa ASEAN

Rais wa Marekani Joe Biden akihutubia viongozi wa mataifa ya ASEAN
Rais wa Marekani Joe Biden akihutubia viongozi wa mataifa ya ASEAN

Hayo yakijiri, viongozi wa mataifa ya kusini mashariki mwa Asia – ASEAN, wamefanya mzungumzo hii leo na rais wa Marekani Joe Biden, ambaye amepongeza kuanzishwa kwa ushirikiano kati ya Marekani na ASEAN akisema ni hatua nzuri sana katika kukabiliana na maswala nyeti yanayoukumba ulimwengu kwa sasa.

Ikiwa ni ziara yake ya kwanza kusini mashariki mwa Asia kama rais, Biden amesema kwamba eneo hilo limo katika mipango muhimu ya utawala wake, na kwamba Marekani inaweka bajeti kwa ajili ya ushirikiano huo.

Amesema kwamba ushirikiano huo utafanikiwa kukabiliana vilivyo na maswala kama mabadiliko ya hali ya hewa, afya, usalama, na kuweka hali ya utulivu katika utawala kwa kuzingatia sheria.

Alisema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho nchini Cambodia, kinachohudhuriwa na viongozi wa mataifa 10 ya ASEAN.

Mataifa ya ASEAN yanalenga kuimarisha ushirikiani na viongozi wa mataifa makubwa duniani akiwemo Biden wa Marekani, waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida, Anthony Albanese wa Australia na rais wa Korea kusini Yoon Suk-yeol.

XS
SM
MD
LG