Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 07:30

Marekani kuipa Ukraine msaada wa ziada wa kijeshi wa dola milioni 800.


Msaada wa kijeshi, uliotolewa kama sehemu ya msaada wa kiusalama wa Marekani kwa Ukraine, ukishushwa kutoka kwenye ndege kwenye uwanja wa kimataifa wa Boryspil nje ya Kyiv. Februari 13, 2022. Picha ya Reuters
Msaada wa kijeshi, uliotolewa kama sehemu ya msaada wa kiusalama wa Marekani kwa Ukraine, ukishushwa kutoka kwenye ndege kwenye uwanja wa kimataifa wa Boryspil nje ya Kyiv. Februari 13, 2022. Picha ya Reuters

Marekani Jumatano imesema inatuma huko Ukraine msaada wa kijeshi wa ziada wa dola milioni 800 ambao unajumuisha silaha, zana za kijeshi na msaada wa kiusalama kuisaidia nchi hiyo kujihami dhidi ya mashambulizi ya Russia katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Rais wa Marekani Joe Biden alimuelezea Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuhusu shehena hiyo katika mazungumzo ya simu na baadaye akasema katika taarifa,

“Jeshi la Ukraine lilitumia silaha tulizotoa kukabiliana na madhara makubwa.”

“Wakati Russia inajianda kuongeza mashambulizi yake katika eneo la Donbas, Biden amesema, “ Marekani itaendelea kuipa Ukraine uwezo wa kujihami.”

Biden ameridhia kutuma vifaa zaidi vya kijeshi nchini Ukraine pamoja na helikopta za ziada, baada ya Zelensky kuomba kupitia video silaha zaidi akisema kwamba “uhuru lazima uwe na silaha bora kuliko udikteta. Bila silaha za ziada, hali itageuka kuwa umwagaji damu usio na mwisho ambao utasambaza uzuni, mateso na uharibifu, Zelensky amesema.

XS
SM
MD
LG