Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 10:17

Marekani inasema Assange alihatarisha maisha ya vyanzo vyake vya habari


Mwanzilishi wa WikiLeaks Julian Assange akiondoka mahakama kuu mjini , Uingereza, July 13, 2011. (Reuters)
Mwanzilishi wa WikiLeaks Julian Assange akiondoka mahakama kuu mjini , Uingereza, July 13, 2011. (Reuters)

Waendesha Mashtaka wa Marekani wamesema kwamba mwanzilishi wa WikiLeaks Julian Assange anakabiliwa na mashtaka ya kutaja vyanzo vyake vya habari na wala sio maoni yake ya kisiasa.

Assange anapinga hatua ya waendesha mashtaka kutaka kumsafirisha kutoka Uingereza anakozuiliwa, hadi Marekani ili kujibu mashtaka hayo.

Waendesha mashtaka wa Marekani wanataka Assange, mwenye umri wa miaka 52 kuletwa Marekani na kujibu kesi ya kuchapisha nyaraka za siri za jeshi la Marekani na mawasiliano ya kidiplomasia.

Wanadai kwamba uchapishaji wa taarifa hizo za siri ziliyaweka hatarini maisha ya wafanyakazi wao na kwamba hakuna sababu ya msingi kuthibitisha hatua ya mchapishaji wanayosema ni uhalifu.

Mawakili wa Assange wameiambia mahakama kwamba kesi dhidi yake ni ya kisiasa na kwamba analengwa kwa kufichua uhalifu wa hali ya juu na kwamba aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump alikuwa ameomba kujua njia mbadala za kumuua.

Forum

XS
SM
MD
LG