Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield alitoa tangazo hilo katika hotuba yake kwa Baraza la Mahusiano ya nje, akiitaja kuwa ni ufuatiliaji wa tangazo la Rais wa Marekani Joe Biden miaka miwili iliyopita kwamba Marekani inaunga mkono kupanua chombo hicho cha wanachama 15.
Wakati Afrika ina viti vitatu visivyo vya kudumu katika Baraza la Usalama, hiyo hairuhusu nchi za Afrika kutoa manufaa kamili ya ujuzi na sauti zao, alisema.
Forum