Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:09

Marekani imeshambulia kambi za Al-shabaab, Somalia


wanajeshi wa umoja wa Afrika wanaopambana na Al-shabaab, Somalia
wanajeshi wa umoja wa Afrika wanaopambana na Al-shabaab, Somalia

Marekani imetekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya wapiganaji wa Al-Shabaab nchini Somalia.

Hayo ni kulingana na kamandi ya kijeshi ya Marekani Afrika, ambayo imeeleza kwamba shambulizi hilo la Ijumaa liliharibu silaha na vifaa vilivyokuwa vimenyakuliwa na al-shabaab.

Ripoti hiyo haijaeleza mahali al-shabaab walikuwa wameiba silaha zilizoharibiwa.

Shambulizi hilo limetekelezwa karibu na kambi ya kikosi cha jeshi la Umoja wa Afrika, katika eneo la Bulo Marer.

Shambulizi limetekelezwa kwa ushirikiano wa serikali ya Somalia na kikosi cha jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia.

Hakuna raia aliyejeruhiwa au kuuawa.

Museveni amezungumzia vifo vya wanajeshi wa Uganda

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameliambia taifa kwamba kuna wanajeshi wa Uganda waliofariki kufuatia shambulizi la kundi la Al-shabab dhidi ya kambi ya jeshi la Uganda nchini Somalia, Ijumaa.

Bila ya kusema idadi ya wanajeshi waliofariki au kujeruhiwa, Museveni ametuma salaam za rambirambi kwa taifa na familia za wanajeshi waliofariki na kuongezea kwamba uchunguzi unaendelea kubaini kilichotokea.

Taarifa ya Museveni ni ya kwanza kutoka kwa afisa wa ngazi wa juu wa serikali tangu tukio hilo.

Tangu mwaka 2006, kundi la Al-shabaab limekuwa likipigana kutaka kuuangusha utawala wa Somalia, unaoungwa mkono na mataifa ya Magharibi, kwa lengo la kutaka kusimika utawala kiislamu wenye msimamo mkali.

Museveni amesema kwamba baadhi ya wanajeshi wa Uganda waliingiwa na wasiwasi wakati wa shambulizi la al-Shabaab na kushindwa kutekeleza wajibu wao vyema, hali iliyopelekea wapiganaji wa al-Shabaab kuharibu silaha za wanajeshi hao na kuwazidi nguvu wanajeshi wa Uganda, waliokimbilia kwenye kambi nyingine, umbali wa kilomita tisa.

Kundi la al-Shabaab limedai kwamba shambulizi lake la kujitoa mhanga liliua wanajeshi 137 wa Uganda. Madai ya idadi ya vifo hayajathibitishwa.

Forum

XS
SM
MD
LG