Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 13, 2025 Local time: 21:03

Mattis: 'Marekani Haiko Iraq Kunyang'anya Mafuta'


Waziri wa Ulinzi Jim Mattis (L) anapokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Iraq Erfan al-Hiyali katika ziara yake Baghdad
Waziri wa Ulinzi Jim Mattis (L) anapokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Iraq Erfan al-Hiyali katika ziara yake Baghdad

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Jim Mattis amesema Jumatatu kuwa Marekani haina nia ya kuchukua mafuta ya Iraq.

Kauli hiyo imekuja baada ya Rais Donald Trump siku za nyuma alipokuwa akitetea kuwa mafuta ya nchi hiyo ni “ngawira” kwa kile jeshi la Marekani inachofanya Iraq na pia ilistahili kuyazuia ili kundi la Islamic State lisipate fursa ya kuyauza.

Mattis ameongea na waandishi waliokuwa wako safarini pamoja na yeye huko Iraq katika ziara yake ya ghafla, ambayo imekuja siku ya pili tangu shambulizi la kijeshi lianze kulisukuma kundi la Islamic State kutoka upande wa magharibi ya mji wa Mosul.

“Nafikiri sote hapa katika chumba hiki, wote tuliyopo Marekani, kwa ujumla tumekuwa tukilipa gharama zetu za gesi na mafuta siku zote, na nina uhakika kwamba tutaendelea kufanya hivyo siku za usoni,” Mattis amesema. “Hatuko Iraq kunyang’anya mafuta ya mtu yoyote.”

Kusimama kwake Iraq katika safari yake ilihusisha kufanya mikutano na Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi na watu viongozi wengine, pamoja na kukutana na Luteni Jenerali Stephen Townsend, ambaye anaongoza majeshi ya ushirika wa magharibi yanayo ongozwa na Marekani ambayo yanashirikiana kulitokomeza kundi la Islamic State.

Mattis anaandaa mpango wake kuharakisha mashambulizi dhidi ya kundi la Islamic State, ambao Trump aliamuru Januari 28 kwamba mkakati huo uwe tayari katika kipindi cha siku thelathini.

Ilivyokuwa shambulizi la Mosul limeanza Jumapili, Mattis amesema nafasi ya Marekani ni ile ile ya kuendesha mashambulizi ya angani na kutoa ushauri kwa vikosi vya Iraqi, na kuwa haitabadilika.

XS
SM
MD
LG