Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 30, 2024 Local time: 02:42

Marekani haijaweka wazi kuipatia Ukraine mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga


Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin hakuthibitisha au kukanusha ripoti kwamba Marekani, inatuma mfumo mwingine wa ulinzi wa makombora ya ardhini mpaka angani wa Patriot nchini Ukraine.

Hii ni baada ya washirika kutoka mataifa takriban 50 kukutana kuratibu uungaji mkono kwa Kyiv katika mkutano ulioangazia masuala ya ulinzi wa angani.

“Ninachowaambia ni kwamba hakutakuwa na mabadiliko katika utangazaji wetu wa mifumo ya Patriot nchini Poland, amewaambia waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika katika makao makuu ya NATO baada ya mkutano wa 23 wa mawasiliano ya ulinzi ya Ukraine.

Kundi la UDCG, ambao ni muungano wa takriban mataifa 50 ambayo yanaratibu msaada wa kijeshi kwa Kyiv katika mapambano yake dhidi ya uvamizi wa Russia.

Gazeti la New York Times na The Associated Press wameripoti mapema wiki hii kwamba Marekani inatoa mfumo mwingine wa Patriot, ikitoa mfano wa maafisa wa ulinzi ambao hawakutajwa kuzungumzia hatua hiyo

Forum

XS
SM
MD
LG