Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 17:31

Marekani: Derek Chauvin ahukumiwa zaidi ya miaka 20 jela kwa kukiuka haki za Floyd


Derek Chauvin akiwa mahakamani katika mji wa Minneapolis, June 25, 2021.
Derek Chauvin akiwa mahakamani katika mji wa Minneapolis, June 25, 2021.

Derek Chauvin, afisa wa zamani wa polisi katika mji wa Minneapolis ambaye alipatikana na hatia ya mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd, amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 20 jela Alhamisi kufuatia mashtaka yaliyofunguliwa na serikali kuu ya Marekani, dhidi yake.

Chauvin ambaye ni mzungu, mwezi Disemba mwaka jana alikiri makosa ya kukiuka haki za kiraia za Floyd, mmarekani mweusi mwenye umri wa miaka 46, alipomkamata mwezi Mei mwaka wa 2020 kwa madai kwamba alitumia noti bandia ya dola 20 kwa kununua tumbaku.

Chauvin tayari anatumika kifungo cha miaka 22 na nusu baada ya kukutwa na hatia ya mashtaka ya serikali ya jimbo juu ya mauaji ya Floyd, mauaji ambayo yalichochea maandamano makubwa dhidi ya ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi kote nchini Marekani.

Hukumu ya serikali ya jimbo na hukumu hiyo ya serikali kuu zitatekelezwa kwa wakati mmoja, lakini Chauvin ataruhusiwa kutumikia kifungo chake katika gereza la serikali kuu badala ya kuendelea kutumukia kifungo katika gereza la serikali ya jimbo la Minnesota, ambako alikuwa amefungwa katika chumba cha peke yake.

Waendesha mashtaka wa serikali kuu walikuwa wanataka apewe kifungo cha miaka 25. “ Alijua kwamba alichokuwa akifanya si sahihi na alikifanya hata hivyo,” naibu mwendesha mashtaka LeeAnn Bell ameimbia mahakama.

“Kwa kweli sijuwi kwa nini ulifanya ulichofanya,” Jaji wa mahakama ya wilaya Paul Magnuson amesema akitoa hukumu ya miezi 252 kwa kuondoa miezi 7 Chauvin aliyokwisha tumikia.

“Lakini uliweka goti lako kwenye shingo la mtu mwingine hadi akafariki, si sahihi,” Magnuson amesema.

“Lazima uadhibiwe vya kutosha,” ameongeza.

XS
SM
MD
LG