Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 10:49

Maporomoko ya ardhi yameua watu waliokuwa katika mazishi Cameroon


Waokoaji wakijitayarisha kubeba miili ya watu waliokufa kutokana na maporomoko ya ardhi Nov. 27, 2022.
Waokoaji wakijitayarisha kubeba miili ya watu waliokufa kutokana na maporomoko ya ardhi Nov. 27, 2022.

Watu 14 wamefariki kutokana na maporomoko ya ardhi katika mji mkuu wa Cameroon, Younde.

Gavana wa mji huo Naseri Paul Bea, amethibitisha tukio hilo akisema kwamba juhudi za uokoaji zinaendelea.

Darzeni ya watu walikuwa wanahudhuria mazishi katika uwanja wa mpira ulio karibu na muinuko wa ardhi kiasi cha mita 20, wakati ardhi hiyo ilipoporomoka na kuwafunika.

Younde ni mojawapo ya miji yenye unyevuunyevu mkubwa Afrika, na wenye milima mingi.

Mvua kubwa imesababisha mafuriko makubwa kote Cameroon, na kuharibu miundo msingi huku ikipelekea maelfu ya watu kukosa makao.

XS
SM
MD
LG