Vyanzo vya usalama ambavyo vinafuatilia hali hiyo vinasema mapigano yameshirikisha vikosi vya serekali na Al Shabab baada ya shambulizi la wanamgambo hao.
Kwa mujibu wa afisa mmoja wa usalama aliyehusika katika makabiliano na Al Shabab, anasema wanamgambo hao walivamia kambi ya kijeshi alfajiri.
Kambi hiyo hutumiwa na vikosi vinavyopewa mafunzo na Eritrea, na wapiganaji wa huko.
Amesema wanamgambo walifanikiwa kuingia kambini na kuondoa magari matatu.
Baada ya wanamgambo kutoka katika mji, oparesheni kutoka mji wa el-Dheer ulioko kaskazini mwa Masagaway ilianza kwa kuwavamia wanamgambo wa Al Shabab na mapambano makali kuanza.
Forum