Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 21:38

Mapigano yanaendelea Sudan, umoja wa mataifa unataka mazungumzo kufanyika


Wapiganaji wa Kikosi cha kijeshi cha RSF wakiwa mjini Khartoum April 23, 2023
Wapiganaji wa Kikosi cha kijeshi cha RSF wakiwa mjini Khartoum April 23, 2023

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan amerejea wito wake kwa pande zinazopigana nchini Sudan kuacha vita na kufanya mazungumzo ya kweli.

Volker Perthes, ambaye amehamia kwa muda huko Port Sudan kwasababu ya kuongezeka mapigano mjini Khartoum, amesema kuna juhudi zinazoendelea kufanikisha mazungumzo kati ya wawakilishi wa jeshi na kikosi cha wapiganaji wa RSF kwa ajili ya kumaliza mapigano hayo.

Perthes amesema kwamba anaendelea kufanya mazungumzo na viongozi wa jeshi la Sudan na wale wa kikosi cha RSF.

Ametoa wito kwa pande zote zinazopigana kuruhusu mashirika ya misaada kuwafikia raia na kuwapatia huduma.

Amesema kwamba kufikia sasa, hakuna mazungumzo ya moja kwa moja yamefanyika kati ya viongozi wa pande mbili, lakini kuna matayarisho ya kufanyika kwa mazungumzo hayo.

Ameeleza kwamba kuna nchi za kikanda na kimataifa zinazoshinkiza mazungumzo kufanyika.

XS
SM
MD
LG