Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:13

Mapigano yanaendelea Sudan huku Marekani ikiwawekea vikwazo wanaohujumu demokrasia


Moshi ukipaa angani kutokea makao ya watu kutokana na mapigano mjini Khartoum. April 30, 2023 PICHA: AFP
Moshi ukipaa angani kutokea makao ya watu kutokana na mapigano mjini Khartoum. April 30, 2023 PICHA: AFP

Mapigano makali yameripotiwa yanaendelea karibu na mji mkuu Khartoum nchini Sudan, licha ya pande mbili zinazopigana kutangaza sitisho la mapigano.

Jeshi la Sudan, na kikosi cha jeshi cha dharura RSF, wanaonekana kujaribu kupata udhibithi wa mji mkuu wa Khartoum na sehemu kuzunguka ikulu ya rais pamoja na makao makuu ya jeshi.

Rais wa Marekani Joe Biden, amesikitishwa na kuendelea kwa ghasia na hivyo kutangaza vikwazo vya kifedha dhidi ya watu wanaovuruga demokrasia nchini Sudan.

Mali zao zenye ushirikiano na benki za Marekani zimefungiwa.

Biden amesema kwamba machafuko yanayoendelea Sudan ni janga baya sana na usaliti mkubwa kwa watu wa Sudan wanaotaka serikali ya kiraia na kipindi cha mpito kuelekea katika demokrasia.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres ameziomba pande zinazopigana Sudan kuacha mapigano na jumuiya ya kimataifa kutoa msaada kwa watu wa Sudan, ambao amesema wanakumbana na hali ngumu ya kibinadamu.

XS
SM
MD
LG