Mapigano mapya kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 yalizuka siku ya Jumapili karibu na mji wenye wakazi wengi mashariki mwa jimbo la Kivu Kaskazini, ambako waasi wanaendesha shughuli zao, jeshi na M23 walisema.
M23 waliteka mji wa Kirumba, kitovu cha kiuchumi cha eneo la Lubero nchini Congo, mwishoni mwa mwezi Juni. Pia waliteka mji jirani wa Kanyabayonga wakati huo huo.
Msemaji wa M23 Willy Ngoma alisema vikosi vya serikali vilishambulia maeneo kadhaa ya waasi karibu na Kirumba mapema Jumapili asubuhi na kwamba mapigano yanaendelea.
Jeshi katika taarifa yake liliripoti mapigano na M23 katika kijiji cha Kikuvo, takriban kilomita zaidi ya kumi kutoka Kirumba.
Forum