Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:47

Mapigano makali yarindima katikati mwa Khartoum

Wanajeshi wa vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) huko Khartoum tarehe 23 Aprili 2023. Picha na Rapid Support Forces/ AFP.
Wanajeshi wa vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) huko Khartoum tarehe 23 Aprili 2023. Picha na Rapid Support Forces/ AFP.

Mapigano makali yanaweza yalisikika katikati mwa Khartoum siku ya Alhamisi wakati jeshi lilipojaribu kuwarudisha nyuma Wanajeshi wa kikosi cha RSF kutoka maeneo karibu na Ikulu ya rais na makao makuu ya jeshi, huku usitishaji wa mapigano wa kudumu ukionekana kuwa mgumu.

Kila upande unaonekana kupigania udhibiti wa eneo katika mji mkuu kabla ya mazungumzo yoyote yanayowezekana ingawa viongozi wa pande zote mbili wameonyesha nia ndogo ya umma kufanya mazungumzo baada ya zaidi ya wiki mbili za mapigano.

Mashambulizi makubwa ya mabomu pia yalisikika katika miji inayopakana ya Omdurman na Bahri. Pande zote mbili zilikuwa zimekubaliana kusitisha mapigano kwa siku saba, jambo ambalo limekiukwa.

“Tangu jana jioni, na asubuhi ya leo, kuna mashambulizi ya anga na sauti za mapigano," alisema Al-Sadiq Ahmed, mhandisi mwenye umri wa miaka 49 akizungumza kutoka Khartoum.

Tumeingia katika hali ya taharuki wa kudumu kwa sababu vita viko karibu na vituo vya vitongoji vya makazi. Hatujui jinamizi hili na hofu itaisha lini.

XS
SM
MD
LG