Waasi wa M23 wameshambulia kambi kadhaa za jeshi la serikali, huku mamia ya watu wakikimbilia Uganda kama wakimbizi.
Mapigano yameendelea mwezi mmoja baada ya viongozi wa jumuiya ya Afrika mashariki kukutana Nairobi, Kenya na kutoa amri kwa kundi la M23 na makundi mengine ya waasi kuacha vita au wakabiliwe kwa nguvu za kijeshi.
Maamuzi ya kushambulia makundi ya waasi kijeshi, yalifikiwa na maraias Uhuru Kenyatta wa Kenya, Felix Tshidekedi wa DRC, Evariste Ndayishimiye wa Burundi na Yoweri Museveni wa Uganda.
Viongozi hao hata hivyo hawajatuma muungano wa jeshi kukabiliana na waasi hao.
Wanajeshi wa Umoja wa mataifa MONUSCO, wamekuwa wakisaidia jeshi la DRC kukabiliana na waasi hao wa M23.