Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:03

Mapigano makali yanaendelea kati ya Israel na makundi ya wapalestina katika ukanda wa Ghaza


moto kutokana na mashambulizi ya roketi katika ukanda wa Ghaza
moto kutokana na mashambulizi ya roketi katika ukanda wa Ghaza

Jeshi la anga la Israel, na wanamgambo wa Palestina, wamepambana kote ukanda wa ghaza mapema hii leo Alhamisi, huku makabiliano yakitokea kwa mara nyingine katika sehemu hiyo takatifu zaidi ya Jerusalem.

Makabiliano hayo yanahofiwa kuharibu kabisa hali ya usalama katika sehemu hiyo n akupelekea hali kukaribia na ilivyokuwa wakati wa vita vibaya vya mwaka uliopita huko ukanda wa Gaza. Machafuko katika eneo la Gaza yamesababishwa na mzozo kati ya Polisi wa Israel na raia wa Palestina mjini Jerusalem.

Mapigano yameongezeka mpakani tangu kutokea mapigano yam waka uliopita yaliyodumu siku 11. Shambulizi la roketi lililovurumishwa kutoka Gaza wiki hii, liliharibu hali ya utulivu iliyokuwa imeshuhudiwa kwa muda wa miezi kadhaa.

Wapiganaji wa Palestina walirusha roketi mbili kutoka Gaza, kuelekea Israel, jumatano jioni na mapema alhamisi, huku ndege ya kivita ya Israel ikitekeleza mashambulizi katika ngome inayokaliwa na kundi la Hamas.

Jeshi la Israel limesema kwamba shambulizi jingine la roketi limepiga sehemu ya mji wa kusini mwa Sderot, ndani ya Israel, na jingine kuangukia Gaza.

XS
SM
MD
LG