Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 23:04

Mapato kutokana na utalii Kenya yaliongezeka theluthi moja mwaka 2023


Mfano wa mbuga za utalii Kenya
Mfano wa mbuga za utalii Kenya

Kenya imekuwa kituo kikuu cha utalii Afrika Mashariki kiasili kinavutia wageni duniani kote kwenye mbuga za wanyamapori

Mapato kutokana na utalii nchini Kenya yaliongezeka karibu theluthi moja mwaka 2023 dhidi ya mwaka uliopita na kuvuka idadi ya mapato kabla ya janga la COVID, kulingana na wizara ya utalii.

Kenya imekuwa kituo kikuu cha utalii Afrika Mashariki kiasili kinavutia wageni kutoka duniani kote kwenye mbuga zake za wanyamapori na fukwe za Bahari ya Hindi. Ripoti ya wizara ya utalii ambayo shirika la habari la AFP imeiona leo Jumapili ilisema mapato yalipanda kwa asilimia 31.5 mwaka jana na kufikia kairbu dola bilioni 2.7.

Lakini matumizi ya kila mtu kwa dola yaliyofanywa na wageni milioni 1.95 yalishuka. Licha ya ongezeko la idadi ya wageni mwaka 2023 ikilinganishwa na mwaka 2022, wastani wa matumizi ya kila mtu kwa dola za Marekani yalipungua kwa kiasi kikubwa, ripoti hiyo ilisema.

Hii kwa kiasi inahusishwa na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Kenya dhidi ya sarafu kuu.

Forum

XS
SM
MD
LG