Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:20

Mkenya anayetafutwa na Marekani akamatwa Nairobi


Pembe za ndovu zilizokuwa zimekamatwa nchini Kenya ambazo ziliteketezwa Aprili 28, 2016.
Pembe za ndovu zilizokuwa zimekamatwa nchini Kenya ambazo ziliteketezwa Aprili 28, 2016.

Vyombo vya usalama mjini Mombasa vimemkamata Mansur Mohamed Surur, maarufu “Mansour”, raia wa Kenya na mtoro aliyekuwa akitafutwa na Marekani.

Surur inasemekana alikuwa anatafutwa na vyombo kadhaa vya usalama kwa kujihusisha na kusafirisha dawa za kulevya na biashara haramu ya pembe za ndovu na faru, ambao ni wanyama wanaoandwa na majangili, pembe hizo zina thamani ya dola milioni 7.

Uhalifu huo unaelezewa kuwa ulihusisha ujangili wa zaidi vifaru 35 na zaidi ya tembo 100.

Alikuwa kati ya raia 47 wa Kenya waliokwama Yemen wakirejea nyumbani kwa ndege ya Skyward Express iliyokodishwa na kuwasili mapema Jumatano asubuhi.

Maafisa wa vyombo kadhaa vya usalama walimpeleka katika kituo cha polisi cha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi.

“Leo majira ya alfajiri… mmiliki wa hati ya kusafiria namba A2283881 na kitambulisho namba 0069184 ambaye alikuwa anatafutwa nchini Marekani kwa makosa yanayo husiana na ujangili wa pembe za ndovu na faru alikamatwa alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi... Hatimaye amekabidhiwa kwa Polisi wa Kimataifa Interpol Nairobi kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria,” ripoti ya polisi juu ya kukamatwa huko imeeleza.

XS
SM
MD
LG