Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 01:14

Maandamano makubwa yafanyika Iran kupinga kunyongwa kwa Wakurdi


Wapiganaji wa Kikurdi wa Peshmerga wanaohusishwa na wale wa Iran wa Kurdistan Freedom Party. Picha ya maktaba.
Wapiganaji wa Kikurdi wa Peshmerga wanaohusishwa na wale wa Iran wa Kurdistan Freedom Party. Picha ya maktaba.

Biashara pamoja na maduka kwenye miji kadhaa katika eneo lenye Wakurdi magharibi mwa Iran zilifungwa Jumanne kutokana na maandamano yalioitishwa ili kupinga kunyongwa siku moja awali, kwa wakurdi wanne waliotuhumiwa kushirikiana na Israel, wanaharakati wamesema.

Wanne hao walikamatwa Julai 2022 na walinyongwa kwenye jela iliyopo kwenye mji wa Karaj, nje kidogo ya Tehran, huku makundi ya kutetea haki za binadamu yakisema kwamba hukumu dhidi yao ilikuwa yenye uonevu.

Kulingana na wanaharakati, mauaji hayo yamezua wasi wasi wa kuongezeka kwa watu kunyongwa nchini Iran, ambako takriban watu wawili wamekuwa wakinyongwa kila siku mwezi huu.

Kundi la kutetea haki za wa Kurdi lenye makao yake Norway la Hengaw, pamoja na lile lenye makao yake Ufaransa la Kurdistan Human Rights Network, walichapisha picha zikionyesha maduka yakiwa yamefungwa kwenye miji kadhaa ikiwemo Kermanshah, Saqez na Sanandaj.

Forum

XS
SM
MD
LG