Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:38

Mamlaka nchini Indonesia imeongeza tahadhari ya juu kwa volcano


Mlima Semeru ukionekana kutoka wiaya ya Lumajang mashariki mwa jimbo la Java Indonesia, Jumamosi Desemba. 18, 2021.
Mlima Semeru ukionekana kutoka wiaya ya Lumajang mashariki mwa jimbo la Java Indonesia, Jumamosi Desemba. 18, 2021.

Mamlaka nchini Indonesia imeongeza tahadhari ya juu kwa volcano iliyo juu zaidi katika kisiwa cha Java, ikisema Mlima Semeru unaweza kulipuka tena baada ya mlipuko wa ghafla mapema mwezi huu

Mamlaka nchini Indonesia imeongeza tahadhari ya juu kwa volcano iliyo juu zaidi katika kisiwa cha Java, ikisema Mlima Semeru unaweza kulipuka tena baada ya mlipuko wa ghafla mapema mwezi huu ambao ulisababisha vifo vya watu 48 na 36 kupotea katika vijiji vilivyozikwa kwenye matope ya volcano.

Shirika la Jiolojia la Indonesia linasema liligundua hali inayoongezeka ambayo inaweza kusababisha maporomoko makubwa ya lava na gesi ya moto sawa na mlipuko wa Desemba 4, ambao ulitanguliwa na mvua kubwa ya masika ambayo iliporomosha mlima wa lava.

Waziri wa nishati alisema kuwa tani za mchanga zilizotolewa na volcano ziliziba mto kwenye njia ya mtiririko wa lava, ambayo inaweza kutishia maeneo yanayozunguka.

XS
SM
MD
LG