Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:24

Mamilioni ya watu kote duniani wamuaga Malkia Elizabeth II

Wananchi wakitoa heshima zao wanapohudhuria Maandamano ya jeneza kutoka Westminster Abbey hadi Wellington Arch jijini London mnamo Septemba 19, 2022. PAUL ELLIS/REUTERS.
Wananchi wakitoa heshima zao wanapohudhuria Maandamano ya jeneza kutoka Westminster Abbey hadi Wellington Arch jijini London mnamo Septemba 19, 2022. PAUL ELLIS/REUTERS.

Mamilioni ya watu kote duniani wamemuaga Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza kwa kufuatilia maziko yake kupitia Televisheni na mitandao ya kijami huku wengi wakikusanyika katika ubalozi wa Uingereza katika miji mikuu mbali mbali. 

Huko London kwenyewe maelfu ya watu walijipanga kando ya njia ambayo jeneza la Malkia ilipita kuelekea kasri ya Winsdor ambako maziko yanafanyika kwa faragha na kuhudhuriwa na familia ya Ufalme na baadhi ya maafisa wa serikali.

Jeneza la Malkia Elizabeth limepita katika njia muhimu kuanzia Kanisa la Westminster Abey hadi mahala anapozikwa baada ya ibada ya kusisimua iliyohudhuriwa na viongozi wa dunia familia na watu 2,000 waliochaguliwa kuwakilisha jamii mbali mbali za Uingereza.

Ibada hiyo ambayo ni ya kihistoria ilikua inasifu miaka 70 ya utawala wake akiwa kiongozi wa kifalme aliyetawala kwa muda mrefu.

Jeneza lake linaongozwa na gwaride la kijeshi huku familia yake ikiwa nyuma yake huku watu wakirusha mauwa wengi wakionekana kuwa na majonzi wakati gari lililokua na jeneza lilipokua linapita.

Mwili wake ulipita katika Kasri ya Buckingham kwa mara ya mwisho ambako kulifanyika sherehe ya kitamaduni na Mfalme Charles kutoa heshima zake za mwisho hadharani kwa mamake.

Ibada ya mwisho katika mazishi ya Malkia ya Elizabeth wa pili inafanyika hivi sasa kwenye kanisa la St. George kwenye kasri ya Winsodr ambako atazikwa.

XS
SM
MD
LG