Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 01:10

Mamia waandamana Senegal kutaka uchaguzi


Mamia kadhaa ya watu wameandamana mjini Dakar, Jumamosi wakimtaka rais kupanga tarehe ya kumchagua mrithi wake kabla ya muhula wake kumalizika tarehe 2 Aprili.

Rais Macky Sall, amekabiliwa na mzozo tangu alipoahirisha uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika Februari 25, na kusababisha mzozo mbaya zaidi wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Baraza la katiba lilibatilisha ucheleweshaji huo na kutaka wiki iliyopita uchaguzi ufanyike haraka iwezekanavyo.

Lakini rais Sall anaonekana hana mpango wa kutekeleza shauri hilo kwa haraka. Ameahirisha uamuzi wa tarehe hiyo hadi atakapozungumza na watendaji wa kisiasa na kijamii kuanzia Jumatatu.

Alhamisi usiku alisema kwamba alitarajia kufikia makubaliano itakapofika Jumanne jioni. Kwa mujibu wa rais Sall, alichelewesha uchaguzi kwa sababu ya mizozo ya kunyimwa sifa za wagombea na wasiwasi wa kurejea machafuko ya 2021 na mwaka jana.

Forum

XS
SM
MD
LG