Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 26, 2024 Local time: 20:44

Mamia waandamana Argntina kupinga sera ya kuokoa uchumi


Mamia ya maafisa wa usalama walifyatua gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kwa waandamanaji katika ghasia za Buenos Aires, Argentina, waliokuwa wakiandamana Jumatano kupinga mapendekezo ya mageuzi ya kiuchumi kwa mujibu wa waandishi wa habari wa AFP.

Magari mawili yalichomwa moto na waandamanaji waliokuwa na hasira baada ya kugeuka kuwa ya vurugu huku wabunge wa Argentina wakijadili mageuzi yaliyopendekezwa na Rais Jabier Milei, kupunguza bajeti.

Ghasia zilizuka kwa mara ya kwanza wakati waandamanaji walipojaribu kukwepa uzio uliowekwa kati yao na Bunge, huku waandamanaji wakiwashambulia kwa mawe maafisa hao.

Waangalizi na wabunge wa upinzani wamesema mamia ya waandamanaji na wabunge wachache walipatiwa matibabu.

Takriban wabunge watano wa upinzani waliokuwepo kwenye umati wa watu walipelekwa hospitalini mbunge Cecilia Moreau, ameambia AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG