Kulingana na ripoti ya shirika linalofuatilia haki za kibinadamu la human rights watch, karibu wanaume 300 wanaaminika kuuawa kwa kupigwa risasi kati ya tarehe 27 na 31 mwezi Machi, katika mji wa Moura, wenye wakaazi karibu 10,000.
Mji huo umeingiliwa na wapiganaji wa kiislamu.
Walionusurika kuuawa walisema kwamba mamluki wanaoaminika kutoka Russia walishiriki katika mauaji hayo yaliyosababisha shutuma kali kutoka kote duniani na kupelekea Umaoja wa mataifa kuanzisha uchunguzi.
Mali imekanusha madai ya kusimamisha oparesheni hiyo katika mji wa Moura na imesema kwamba itafanya uchunguzi wake.
Msemaji wa umoja wa mataida Seif Magango amesema kwamba huenda zaidi ya watu 500 waliuawa.
Kuna ripoti kwamba wanajeshi walinajisi wanawake na kuiba mali.