Mwendesha mashtaka wa mahakama ya kijeshi ambaye ameanzisha uchunguzi huo kwa agizo la wizara ya ulinzi, alitembelea kituo cha Gossi mashariki mwa nchi hapo tarehe 23 Aprili.
Taarifa rasmi imesema “atatafuta ukweli wa ushahidi wote” wa kesi hiyo na atawafahamisha wanainchi kikamilifu.
Tarehe 21 Aprili, siku mbili baada ya wanajeshi wa Ufaransa kuikabidhi tena kambi hiyo kwa Mali, walitoa video inayosemekana inawaonyesha mamluki wa Russia wakizika maiti karibu na kambi hiyo ili kuwashtumu kwa uwongo wanajeshi wa Ufaransa wanaoondoka.
Katika video hiyo iliyorekodiwa na ndege isiyo na rubani, wanajeshi wa Russia wanaonekana wakifunika maiti na mchanga karibu na kambi ya Gossi.
Ufaransa ilikabidhi rasmi udhibiti wa kambi ya Gossi kwa Mali Jumanne iliyopita kama sehemu ya mchakato wa kuwaondoa wanajeshi wa Ufaransa uliotangazwa mwezi Februari.