Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 20:32

ICC:Tunaifuatilia Mali kwa karibu


Wapiganaji kutoka kundi la Ansar Dine wakiwa katika eneo moja la soko huko Timbuktu, Mali
Wapiganaji kutoka kundi la Ansar Dine wakiwa katika eneo moja la soko huko Timbuktu, Mali

Ripoti ya ofisi ya mwendesha mashtaka ya ICC inasema itaamua karibuni kama ianzishe uchunguzi dhidi ya Mali

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC inasema inafuatilia kwa karibu hali nchini Mali na itatathmini kwa kina kama uhalifu wa vita, uhalifu dhidi ya binadamu au mauaji ya halaiki yametendeka.

Katika taarifa ya Jumanne ofisi ya mwendesha mashtaka ya ICC ilisema imepokea ripoti kutoka vyanzo kadhaa ikiwa ni pamoja na maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa juu ya mauaji, utekaji nyara, ubakaji na kuandikisha watoto kuwa wanajeshi na makundi mbali mbali huko kaskazini ya Mali.

Haikuwekwa bayana kama shutuma za uhalifu zilifanywa na waasi wa Tuareg na wanamgambo wa ki-Islam ambao karibuni walichukua udhibiti wa kaskazini, au na wanajeshi wa serikali au na pande zote mbili.

Ofisi ya mwendesha mashtaka ilisema itaamua hivi karibuni kama ianzishe uchunguzi.

Wanajeshi waasi walichukua madaraka kwa njia ya mapinduzi hapo Machi 22, na kumshutumu Rais aliyeondolewa madarakani Amadou Toumani Toure kwa kushindwa kutoa vifaa vinavyostahili kwa jeshi ili kushughulikia uasi wa Tuareg huko kaskazini.

Katika kuteka kwao maeneo matatu ya kaskazini, wa-Tuareg walipambana na wanachama wa kundi la ki-Islam lenye msimamo mkali la Ansar Dine.

Waasi wa Tuareg walitangaza uhuru wa eneo la kaskazini, lakini hatua yao ilipingwa na nchi jirani pamoja na Umoja wa Afrika.

Baada ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika magharibi-ECOWAS kuweka vikwazo vikali dhidi ya viongozi waliofanya mapinduzi, baraza la kijeshi lilikubali kuunda serikali ya mpito ili kupanga uchaguzi mpya.

XS
SM
MD
LG