Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:28

Malawi yatupilia mbali wasi wasi wa Marekani kuhusu kampeni ya unyanyasaji dhidi ya mkuu wa kupambana na rushwa


Rais wa Malawi Lazarus McCarthy Chakwera akizungumza katika hafla ya kutia saini katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington.
Rais wa Malawi Lazarus McCarthy Chakwera akizungumza katika hafla ya kutia saini katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington.

Serikali ya Malawi imetupilia mbali wasi wasi wa Marekani kwamba inafanya kampeni ya unyanyasaji dhidi ya mkuu wa kupambana na rushwa.

Ubalozi wa Marekani mjini Lilongwe ulishutumu vikali kile ilichokiita kunyanyaswa kwa Mkurugenzi wa Idara ya Kupambana na Rushwa Malawi, Martha Chizuma. Taarifa hiyo imekuja baada ya serikali kumsimamisha kazi Chizuma kwa malalamiko yake kuhusu kuzuia uchunguzi wake anaoufanya.

Taarifa ya ubalozi wa Marekani ilisema ilikuwa na wasi wasi mkubwa sana na jinsi serikali ya Malawi inavyofanya kazi katika kumnyanyasa mkurugenzi mkuu wa idara ya kumpambana na rushwa nchini humo, Martha Chizuma.

Wiki iliyopita, katibu wa Ofisi ya Rais na Baraza la Mawaziri, Colleen Zamba alimsimamisha kazi Chizuma, akiitaja sauti iliyorekodiwa ambapo Chizuma aliwashutumu baadhi ya maafisa wa juu kuzuia mapambano yake dhidi ya rushwa.

Mahakama iliitaka serikali kuondoa usimamishaji huo, lakini serikali iliitaka mahakama kufuta amri yake.

Katika taarifa iliyorekodiwa, balozi wa Marekani nchini Malawi, David Young alisema hatua ya serikali “ilifikia kilele miezi miwili ya unyanyasaji” dhidi ya Chizuma, alisema ubalozi wake umesikitishwa sana na hatua za serikali.

Young amesema “kama mshirika wa kidemokrasia, ubalozi wa Marekani unaiangalia serikali ya Malawi kwa kujihusisha katika mapambano dhidi ya rushwa na siyo kufanya kampeni ya manyanyaso dhidi ya wale wanaopinga rushwa. Tumejihusisha na maafisa waandamizi wa serikali kuweza kuwepo kwa nia ya dhati katika mapambano dhidi ya ufisadi, lakini juhudi hizo bado hazijaleta matokeo yoyote.”

Balozi Young alielezea kuwa ukamataji wa Chizuma hapo mwezi Desemba na mashtaka ya uhalifu ambayo serikali iliyawasilisha dhidi yake kama mifano mingine ya unyanyasaji wa serikali.

“Nia yetu ya dhati kwa maendeleo ya Malawi inategemea na Imani kwamba Malawi itatumia rasilimali za umma ikiwa ni pamoja na fedha za maendeleo, kwa uwazi, haki na uwajibikaji. Vitendo hivi vya karibuni vinaharibiu uaminifu wa serikali ya Malawi ambayo ilielezewa nia ya dhati kupambana na ufisadi,” amesema Young.

Marekani ni mfadhili mkubwa wa kifedha wa Malawi, ikiipatia zaidi ya dola milioni 350 kwa mwaka kama msaada wa pande mbili.

Kwa mujibu wa kamati ya bajeti na fedha katika bunge la Malawi, utafiti umebaini kwamba asilimia 20 ya bajeti ya taifa ya Malawi inapotea kutokana na rushwa.

Moses Kunkuyu ni msemaji wa serikali ya Malawi, alisema katika taarifa yake kwamba serikali ya Malawi itafuatilia kupitia njia za kidiplomasia kuzungumzia wasi wasi ulioelezewa na Marekani.

Kunkuyu ambaye pia ni waziri wa habari wa serikali, aliiambia radio ya taifa kwamba ni makossa kwa serikali kushindwa kupambana na rushwa.

Alisema Rais Lazarus Chakwera alimuunga mkono Chizuma kwa vile wabunge wa upinzani walipinga uteuzi wake kama mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Rushwa.

“Limekuja suala la sauti, rais alisimama naye na kumsamehe. Halafu tume yauchunguzi ilipendekeza kwamba hatua zaidi zichukuliwe dhidi yake, na rais alisimama naye. Halafu, kumekuwepo na masuala ya kufadhili operesheni ya kudumamaza ACB, rais alihakikisha kwamba serikali yake itoe ufadhili kwa ACB,” alisema Kunkuyu.

Mahakama Kuu ya Malawi ilitupilia mbali ombi la serikal kuondoa zuio dhidi ya kusimamishwa kazi kwa Chizuma na ilisema halina nguvu.

Serikali ya Malawi ilisema kwamba itakata rufaa dhidi ya maamuzi ya Jumatano, ambayo yamemruhusu Chizuma kurejea kazini.

XS
SM
MD
LG