Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 21:10

Malawi yagundua kaburi la halaiki kaskazini mwa nchi hiyo


Rais wa Malawi Lazarus McCarthy Chakwera akizungumza katika hafla katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington
Rais wa Malawi Lazarus McCarthy Chakwera akizungumza katika hafla katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington

Malawi imegundua kaburi la halaiki kaskazini mwa nchi hiyo lenye mabaki ya watu 25 wanaoshukiwa kuwa wahamiaji kutoka Ethiopia, polisi walisema Jumatano.

“Kaburi hilo liligunduliwa Jumanne jioni, lakini tulilizingira na kuanza kufukua leo. Kufikia sasa, tumegundua miili 25," msemaji wa polisi Peter Kalaya aliambia shirika la habari la AFP.

Polisi walitahadharishwa na wanakijiji katika eneo la Mzimba, yapata kilomita 250 kaskazini mwa mji mkuu, Lilongwe, ambao waliona kaburi hilo wakati wakikusanya asali mwitu msituni.

Tunashuku kuwa walikuwa wahamiaji haramu ambao walikuwa wakisafirishwa hadi Afrika Kusini kupitia Malawi," alisema.

Aliongeza kuwa ushahidi uliokusanywa kutoka kwenye eneo hilo ulionyesha waathirika walikuwa wanaume raia wa Ethiopia wenye umri wa kati ya miaka 25 hadi 40.

Miili hiyo iliyoharibika ilitolewa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa uchunguzi zaidi.

XS
SM
MD
LG