Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 16:48

Malawi kuongezwa muda wa mkopo,IMF yasema


Jina la IMF kwenye jengo lake mjini Washington DC
Jina la IMF kwenye jengo lake mjini Washington DC

Shirika la kimataifa la fedha , IMF limesema Jumatatu kwamba Malawi imeomba kuongezewa muda wa mkopo kwa miaka minne zaidi ili kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi inayoendelea kushuhudiwa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, taifa hilo la kusini mwa Afrika limekuwa likishuhudia uhaba kubwa wa fedha za kigeni. Mwezi uliopita serikali ilipunguza dhamani ya kwacha kwa asilimia 25 dhidi ya dola kama hatua ya kupunguza uhaba wa fedha zakigeni.

Ripoti ya Jumatatu kutoka IMF imetolewa baada ya mashauriano kati yake , maafisa wa serikali pamoja na wale kutoka sekta binafsi. IMF imesema kwamba baadhi ya masharti yake kwa Malawi ni kuonyesha uwezo wa kulipa madeni pamoja na kutatua madai ya kutofuchua hifadhi ya fedha za kigeni.

IMF imesema kwamba imekaribisha hatua ya Malawi ya kudhibiti soko la sarafu za kigeni wakati pia ikiomba ushauri kutoka wa wataalam wa mikopo ili kuweka mikakati ya kulipa deni la umma.

XS
SM
MD
LG