Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 08:07

Makundi ya wanaharakati yaonywa Sudan Kusini


Wabunge wa Sudan kusini wakihudhuria kikao mjini Juba kwenye picha ya maktaba
Wabunge wa Sudan kusini wakihudhuria kikao mjini Juba kwenye picha ya maktaba

Makundi ya kutetea haki za vyombo vya habari nchini Sudan Kusini yamelaani matamshi ya mbunge anayesimamia kamati ya habari ambaye alisema, vyombo vya habari vinaweza kufutiwa leseni.

Onyo hilo ikiwa vitaripoti kuhusu matumzi ya bunge, ikiwemo mishahara ya wabunge, bila idhini kutoka kwa Spika wa bunge.

Paul Youane Bonju, mwenyekiti wa kamati ya habari amesema wanahabari wanaweza kushtakiwa iwapo hawatofuatisha utaratibu wa kuripoti juu ya shughuli za kifedha za wabunge.

Bonju ametaja ripoti zilizochapishwa na vyombo vya habari miaka mitano iliyopita kuhusu dola elfu 40 rais Salva Kiir alizowapa wabunge kwa ajili ya posho na mikopo ya gari.

Ripoti kuhusu pesa hizo zilisababisha malalamiko makubwa katika taifa hilo changa duniani, ambapo serikali inadaiwa mishahara na wafanyakazi wengi,pamoja na mshahara wa wastani wa mwalimu ambao ni chini ya dola 400 kwa mwaka.

Vyombo vya habari vinasema matamshi ya Bonju ni jaribio la kuuficha umma habari, wakati Sudan kusini ikijaribu kujenga demokrasia iliyo thabiti.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la maendeleo ya vyombo vya habari nchini Sudan kusini Micheal Duku, amesema wabunge hawawezi kuvizuia vyombo vya habari kuripoti juu ya kazi yao ambayo ni kwa ajili ya maslahi ya umma.

XS
SM
MD
LG