Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 11:49

Makubaliano yamepatikana kuendelea kusafirisha nafaka kutoka Ukraine


Meli iliyobeba nafaka ikiondoka bandari ya Ukraine Oct 31, 2022
Meli iliyobeba nafaka ikiondoka bandari ya Ukraine Oct 31, 2022

Maafisa wa serikali ya Ukraine na Uturuki wamesema kwamba wamefikia makubaliano ya kuendelea kutekeleza mkataba wa usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine kupitia Black Sea kwa muda wa miezi minne zaidi.

Kuongezwa muda kwa makubaliano hayo ni hatua inayojiri wakati makubaliano ya awali yalifikiwa chini ya usimamizi wa Uturuki na Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Julai, yakieleka kufikia muda wake wa mwisho.

Katibu mkuu wa Umoja wa mMtaifa Antonio Guterres amesema kwamba amefurahishwa na hatua hiyo, na kuongezea kwamba ataendelea kuhakikisha kwamba usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine unaendelea vyema.

Katika taarifa, Guterres ameongezea kwamba anaendelea kufanya kazi kuhakikisha kwamba vizuizi vyoye vinavyohusiana na usafirishaji wa chakula na mbolea kutoka Russia, vinaondolewa.

Makubaliano hayo yaliyosainiwa Istanbul, Uturuki, yanalenga kuhakikisha kwamba bei ya chakula na mbolea inashuka ili kuhakikisha kwamba hakuna uhaba wa chakula kote duniani.

XS
SM
MD
LG