Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 12, 2024 Local time: 10:04

Makombora ya Russia yalipiga vituo vya umeme huko Ukraine


Mfano wa makombora yanayosafiri umbali mrefu
Mfano wa makombora yanayosafiri umbali mrefu

Shambulizi hilo la anga lilifanywa na makombora ya masafa ya balistiki na yale yanayosafiri umbali mrefu

Makombora ya Russia yalipiga vituo vya umeme katikati na magharibi mwa Ukraine leo Jumamosi, na kuongeza shinikizo kwa mfumo wa umeme ambao umedhoofika wakati nchi hiyo ikikabiliwa na uhaba wa ulinzi wa anga licha ya maafikiano ya kupatikana kwa msaada wa kijeshi wa Marekani.

Shambulizi la anga, lilifanywa na makombora ya masafa ya balistiki na yale yanayosafiri umbali mrefu yaliyofyatuliwa na walipuaji wa kimkakati wa Russia walio kwenye Artcic Circle, yalikuwa ni mashambulizi ya nne makubwa ya anga yaliyolenga mfumo wa umeme tangu March 22.

“Adui kwa mara nyingine tena ameshambulia vinu vya umeme vya Ukraine,” imesema DTEK, kampuni kubwa sana binafsi ya umeme, na kuongezea kuwa vituo vyake sita vya umeme vimepata uharibifu mkubwa katika mashambulizi ya usiku kucha.

Muonekano wa mkoa wa Ivano-Frankivsk huko Ukraine. June 6, 2021. (REUTERS/Sergiy Karazy)
Muonekano wa mkoa wa Ivano-Frankivsk huko Ukraine. June 6, 2021. (REUTERS/Sergiy Karazy)

Waokoaji walipambana kuzima mioto katika vituo kadhaa katika mikoa ya magharibi ya Lviv na Ivano-Frankivsk, ambayo inapakana na wanachama wa NATO mataifa ya Poland na Romania, maafisa wamesema.

Baada ya mashambulizi kwenye vituo vya nishati katika mkoa wa kati wa Dnipropetrocks, usambazaji wa maji ya bomba ulivurugika, katika mji anakotoka Rais Volodymyr Zelenskyy wa Krvyvyi Rih, maafisa wamesema.

Ulinzi wa anga wa Ukraine ulitungua makombora 21 kati ya 34 yaliyokuwa yameelekezwa huo, kamanda wa jeshi la anga alisema katika taarifa yake.

Forum

XS
SM
MD
LG