Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 13:38

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akubali rasmi uteuzi wa chama cha Demokratik


Makamu wa Rais aliyeteuliwa na chama cha Democratik Kamala Harris akiwasili kuhutubia katika siku ya mwisho ya Kongamano la Kitaifa la chama cha Demokratik Alhamisi, Agosti 22, 2024, Chicago. (AP).
Makamu wa Rais aliyeteuliwa na chama cha Democratik Kamala Harris akiwasili kuhutubia katika siku ya mwisho ya Kongamano la Kitaifa la chama cha Demokratik Alhamisi, Agosti 22, 2024, Chicago. (AP).

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris alikubali rasmi uteuzi wa chama cha Demokratik  kuwa mgombea urais siku ya Alhamisi kukiwa na wito mkubwa  wa kumaliza vita huko Gaza na kupambana na dhuluma kote duniani,   akiweka  tofauti kubwa na mgombea wa Republikan Donald Trump.

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amekubali rasmi

uteuzi wa chama cha Demokratik kuwa mgombea urais siku ya Alhamisi kukiwa na wito mkubwa wa kumaliza vita huko Gaza na kupambana na dhuluma kote duniani, akiweka tofauti kubwa na mgombea wa Republikan Donald Trump.

Katika mapambano ya kudumu kati ya demokrasia na udhalimu,

najua ninaposimama na najua Marekani iko wapi,

Harris alisema akimshutumu Trump kwa kuwasujudia madikteta.

Katika usiku wa mwisho, uliosubiriwa sana katika mkutano wa siku nne huko Chicago, Harris, mwenye umri wa miaka 59, aliahidi kufungua njia mpya kusonga mbele huku yeye na Trump, mwenye umri wa miaka 78 wakiingia katika wiki 11 za mwisho za kampeni zilizo na ukaribu mno.

Forum

XS
SM
MD
LG