Prof. Osinbajo ana matumaini ya kuchukua nafasi inayowachwa wazi na rais wa sasa Muhammadu Buhari, ambaye mhula wake unakamilika mwezi May mwaka ujao.
Osinbajo, ambaye ni wakili, alichaguliwa kama naibu wa Buhari mwaka 2015.
Katika video fupi aliyoweka kwenye mitandao ya kijamii, ameahidi kuboresha hali ya usalama na kujenga uchumi, miundo mbinu, kukabiliana na umaskini pamoja na kufanyia mabadiliko muhimu mfumo wa sheria.
Amemsifu rais Buhari, akimtaja kuwa mzalendo wa kweli wa Nigeria na mchapa kazi wa hakika kwa taifa hilo.
Amesema kwamba utawala wao umeafanya kazi nzuri hasa kuhusu usalama licha ya nchi hiyo kupitia hali ngumu katika historia ya nchi hiyo.