Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:16

Majaribio ya chanjo ya Covid-19 yaonyesha matumaini makubwa


Kijichupa kilichoandikwa "Chanjo ya Virusi vya Corona"
Kijichupa kilichoandikwa "Chanjo ya Virusi vya Corona"

Chanjo ya virusi vya Corona inayofanyiwa uchunguzi na wanasayansi wa chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza inaonyesha kwamba ina nguvu za kuongeza nguvu ya kinga mwilini, kulingana na majaribio ya utafiti wa hatua za awali.

Matokeo yaliyochapishwa Jumatatu katika jarida la madawa la Uingereza, The Lancet, yalionyesha chanjo inayofanyiwa majaribio na kampuni ya madawa ya Astra-Zeneca na chuo kikuu cha OXFORD, ilitoa majibu mazuri kote kwenye seli zinazopambana na maradhi Pamoja na seli muhimu kwenye mfumo wa kinga zijulikanazo kama T-cells.

Majaribio hayo ni sehemu ya hatua ya pili ya uchunguzi wa chou cha Oxford, ambao haukuangalia iwapo chanjo inazuia dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona, swali ambalo litajibiwa kwenye hatua ya tatu ya majaribio ambayo tayari imeshaanza.

Tunahitaji utafiti zaidi ili kubaini iwapo chanjo hii inatoa kinga kamili kwa mtu aliyeambukizwa virusi vya Corona, na iwapo inatoa kinga, ni kwa muda gani, alisema Andrew Pollard, ambaye alitayarisha roipoti kuhusu utafiti wa chuo cha Oxford.

-Imetayarishwa na Mkamiti Kibayasi, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG