Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:24

Mahakama yampata Trump na makosa


Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump. April 23 2022. PICHA: AP
Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump. April 23 2022. PICHA: AP

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, amekutwa na makosa ya kutoheshimu amri ya mahakama, baada ya kushindwa kuwasilisha nyaraka alizotakiwa kuzifikisha katika uchunguzi kuhusiana na biashara zake.

Jaji katika mahakama ya New York, ameamuru Trump kutozwa faini ya dola 10,000 kila siku, hadi atakapoheshimu amri hiyo katika uchunguzi unaofanyika na ofisi ya mwanasheria mkuu wa New York.

Trump alishindwa katika jaribio la kuzuia amri ya kuasilisha nyaraka hizo, na baadaye kukosa kuziasilisha alivyoamuriwa na mahakama. Alikuwa amepewa muda hadi March tarehe 3, ambao uliongezwa hadi March 31 baada ya mawakili wake kuomba mda zaidi.

Mwansaheria mkuu wa New York Letitia James amesema kwamba uchunguzi wake ulibaini kwamba kuna ushahidi wa kutosha kwamba kampuni yake Trump ilikuwa ikitoa taarifa za kifesha za uongo kuhusu thamani ya mali zake ili kujinufaisha kifedha.

Trump amesema kwamba kampuni yake haijafanya makosa yoyote, na ametaja uchunguzi huo kuwa wa kisiasa.

XS
SM
MD
LG