Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 02:13

Mahakama ya Uturuki yaacha kusikiliza kesi ya mauaji ya Khashoggi


Aliyekuwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi PICHA: AP
Aliyekuwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi PICHA: AP

Mahakama ya Uturuki imesitisha kusikilizwa kwa kesi ya raia 26 wa Saudi Arabia, walioshtakiwa kwa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, na kuamuru kwamba kesi hiyo ipelekwe kusikilizwa nchini Saudi Arabia.

Kesi ya mauaji dhidi ya washukiwa hao 26 ilikuwa inasikilizwa bila ya wao kuwepo mahakamani.

Mauaji ya Khashoggi, ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa sana wa ufalme wa Saudi Arabia, yaliushtua ulimwengu, na ripoti ya ujasusi iliyotolewa mwaka uliopita, ilisema kwamba Prince Mohammed bin Salman aliidhinisha mauaji hayo.

Aliuawa mwaka 2018.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mwaka 2020 huku kukiwepo uhusiano mbaya kati ya Uturuki na Saudi Arabia, lakini Uturuki ikaamua kuboresha uhusiano huo kwa sababu ya maslahi ya uchumi wake, ikitafuta kuimarisha uwekezaji zaidi.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa vikali hatua ya Uturuki ya kuipelekea kesi hiyo Saudi Arabia yakiamini kwamba haki haitapatikana.

XS
SM
MD
LG