Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:51

Mahakama ya Paris yatupilia mbali ombi la wanaharakati kuhusu mradi wa mafuta Uganda na Tanzania


Wanaharakati wa mazingira wameshikilia mabango yakipinga mradi wa nishati wa Uganda wakati wa maandamano ya kuingilia kati mkutano wa wanahisa wa TotalEnergies, Paris, Ufaransa, Mei 25, 2022. REUTERS
Wanaharakati wa mazingira wameshikilia mabango yakipinga mradi wa nishati wa Uganda wakati wa maandamano ya kuingilia kati mkutano wa wanahisa wa TotalEnergies, Paris, Ufaransa, Mei 25, 2022. REUTERS

Mahakama moja ya  Ufaransa iliamua Jumanne kwamba kesi iliyoletwa na wanaharakati dhidi ya kampuni kuu ya nishati ya TotalEnergies (TTEF.PA) kuhusu miradi yake ya mafuta nchini Uganda na Tanzania haiwezi kukubalika.

Kwenye kesi iliyowasilishwa mwaka wa 2019, makundi sita ya wanaharakati wa Ufaransa na Uganda yalishutumu kampuni hiyo kwa kutofanya kila iwezalo kulinda watu na mazingira kutokana na shughuli za kampuni ya Tilenga Oil Development na Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki la dola bilioni 3.5.

Wanaharakati hao walitaka mahakama iamuru TotalEnergies kusitisha miradi hiyo ya Afrika mashariki, kwa kuzingatia sheria ya Ufaransa ya mwaka 2017 inayotaka makampuni kutambua hatari za haki za binadamu na mazingira katika shughuli zao za kimataifa na minyororo ya ugavi, na kuchukua hatua za kuzizuia.

Mahakama hiyo ya Paris ilitupilia mbali ombi hilo, ikisema kwamba ni hakimu pekee anayechunguza kesi hiyo kwa kina zaidi ndiye anayeweza kutathmini kama shutuma dhidi ya TotalEnergies zina ukweli na kisha kuendelea na ukaguzi wa shughuli kwenye eneo.

XS
SM
MD
LG