Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 13:46

Mahakama ya Pakistan yasitisha adhabu ya kifungo dhidi ya waziri mkuu wa zamani Imran Khan


Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan wakati wa mahojiano na Reuters mjini Lahore, Pakistan, Machi 17, 2023.
Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan wakati wa mahojiano na Reuters mjini Lahore, Pakistan, Machi 17, 2023.

Adhabu ya kifungo cha waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan kwa hatia ya ufisadi imesitishwa leo Jumanne, wakili wake amesema, lakini haikuwa wazi ikiwa ataachiwa huru.

Msemaji wa chama cha Khan cha Tehreek e-Insaf (PTI) amesema mahakama kuu ya Islamabad ilibatilisha uamuzi wa mahakama ya chini mwezi huu wa kumfunga jela miaka mitatu, hukumu ambayo ilimzuia kugombea uchaguzi ujao.

Chama cha Khan na mawakili wake wamesema ameachiliwa kwa dhamana, lakini wanahofia Khan mwenye umri wa miaka 70 atakamatwa tena kutokana na moja kati ya kesi zaidi ya 200 zinazomkabili tangu alipoondolewa madarakani kwa kura ya bunge mwaka jana.

Khan amekuwa gerezani kwa muda wa wiki tatu tangu Jaji alipomkuta na hatia ya kushindwa kutangaza ipasavyo zawadi alizopokea akiwa madarakani.

Forum

XS
SM
MD
LG