Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:42

Mahakama ya Nairobi imemuachia Mwendwa baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha upande wa serikali


Nick Mwendwa, Rais wa Shirikisho la soka Kenya akifurahia uwamuzi mahakamani
Nick Mwendwa, Rais wa Shirikisho la soka Kenya akifurahia uwamuzi mahakamani

Nick Mwendwa alikamatwa Novemba 12 siku moja baada ya waziri wa michezo kenya, Amina Mohamed kuunda kamati ya muda kusimamia shirikisho la soka la Kenya (FKF) baada ya uchunguzi kufichua madai ya ukiukaji wa sheria wakati wa uongozi wake

Mahakama ya Kenya Alhamis ilitupilia mbali mashtaka ya rushwa dhidi ya mkuu wa shirikisho la soka nchini aliyesimamishwa kazi na kutangaza kuwa kesi hiyo imefungwa baada ya serikali kukosa kutoa ushahidi wowote dhidi yake.

Nick Mwendwa alikamatwa Novemba 12 siku moja baada ya waziri wa michezo kenya, Amina Mohamed kuunda kamati ya muda kusimamia shirikisho la soka la Kenya (FKF) baada ya uchunguzi kufichua madai ya ukiukaji wa sheria wakati wa uongozi wake. Lakini hakimu wa mahakama ya Nairobi, Wandia Nyamu alitupilia mbali kesi hiyo baada ya waendesha mashtaka ambao walikuwa wametuma maombi ya siku saba kuwawezesha kufanya uchunguzi kutaka kufunga faili dhidi ya mshukiwa huyo mwenye miaka 42.

Nick Mwendwa, Rais wa shirikisho la soka Kenya
Nick Mwendwa, Rais wa shirikisho la soka Kenya

Kwa hivyo naamuru suala hili lifungwe Nyamu alisema, pia aliamuru kwamba Mwendwa arejeshewe malipo yake dhidi ya dhamana ya shilingi milioni nne, sawa na dola 35,500. Upande wa Mashtaka hata hivyo, ulisema unapanga kuendelea na uchunguzi kuhusu fedha za FKF baada ya Mohamed kushutumu bodi hiyo kwa kushindwa kujibu pesa zilizopokelewa kutoka kwa serikali na wafadhili wengine.

Kamati ya walezi ya FKF ilikutana na vilabu vya daraja la juu nchini Kenya, jana Jumatano na kutangaza kuanza tena kwa ligi ya nyumbani hapo Disemba 4 baada ya kuahirishwa kwa wiki mbili kwa sababu ya kusimamishwa kwa shirikisho hilo.

XS
SM
MD
LG