Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 01:16

Mahakama ya Marekani yakataa ombi la R.F Kennedy la kuondolewa kwenye karatasi ya kupigia kura


Jengo la Mahakama ya Juu ya Marekani mjini Washington DC.
Jengo la Mahakama ya Juu ya Marekani mjini Washington DC.

Mahakama ya Juu ya Marekani Jumanne imepinga ombi la aliyekuwa mgombea huru wa urais Robert F. Kennedy Jr, la kuondolewa kwenye karatasi ya kura ya majimbo ya Wisconsin na Michigan, kwenye uchaguzi wa Novemba 5.

Kennedy alisema kuwa alikusudia wapiga kura ambao wangemuunga mkono kupeana kura zao kwa mgombea wa Repablikan, rais wa zamani Donald Trump. Mahakama hiyo imekataa kuamuru tume ya uchaguzi ya Wisconsin pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Michigan, Jocelyn Benson, kumuondoa kwenye karatasi ya kura kwenye majimbo hayo.

Michigan na Wisconsin ni miongoni mwa majimbo yenye ushindani wa karibu, na yanayotarajiwa kuamua mshindi kati ya Trump na mgombea wa Repablican, Kamala Harris. Jaji wa Kikonsavative Neil Gorsuch alijiondoa kwenye uamuzi kuhusu kura ya Michigan, lakini hakuna mwingine yeyote aliyejiondoa.

Kennedy ambaye ni wakili wa mazingira na pia mwanaharakati dhidi ya chanjo, na anayefahamika zaidi kama RFK Jr, aliomba Mahakama ya Juu kuingilia kati kwenye juhudi zake za kubaki kwenye karatasi ya kura kwenye baadhi ya majimbo, na kujiondoa kwenye baadhi.

Mwezi uliopita, Mahakama hiyo ilipinga ombi lake la kutaka kurejeshwa kwenye karatasi ya kura ya New York. Kennedy alisitisha kampeni zake Agosti na badala yake kuunga mkono Donald Trump.

Forum

XS
SM
MD
LG