Mahakama ya kijeshi huko Kivu Kusini nchini DRC imemhukumu kifungo cha maisha jela kiongozi wa waasi Congo aliyetuhumiwa kwa kufanya ugaidi katika Hifadhi ya Kitaifa ya Kahuzi-Biega mashariki mwa Congo na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Kulingana na AFP, Chance Mihonya, Kapteni wa zamani wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC), aliondoka kwenye jeshi tangu Julai 2019, alihukumiwa Jumanne jioni na mahakama ya kijeshi ya Kivu Kusini iliyokaa kwenye uwanja huko Katana, pembeni mwa Hifadhi, kiasi cha kilomita 45 kutoka mji mkuu wa jimbo Bukavu.
Mahakama hiyo hiyo kwa upande mwingine ilimwachilia huru kwa kukosa ushahidi wa kutosha mtu ambaye alishukiwa kutoa silaha na risasi kwa kundi la Chance Mihonya, alifafanua Kanali-hakimu Innocent Mayembe, rais wa kwanza wa mahakama ya kijeshi ya jimbo. Chance Mihonya, alikutwa na hatia ya mashtaka yote aliyoshtakiwa, alihukumiwa haswa kwa kuteka nyara na kuwatesa dazeniya wakazi katika vijiji kadhaa vilivyopo katika hifadhi hiyo mnamo mwaka 2019 na 2020 .